Loading...

Nigeria yatwaa medali ya shaba kwenye mashindano ya Olympic.

Nigeria wameshinda medali yao ya kwanza kwenye mashindano ya Olympic mwaka 2016 baada ya kuifunga Honduras mabao 3-2 kwenye mchezo wa kuwania medali ya shaba ambapo Sadiq Umar alifunga mara mbili huku Aminu Umar akifunga bao moja.

Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi, aliyekuwa nahodha wa Nigeria amesema: “Nimefurahishwa na hiki kikosi, vijana walijituma sana.”

“Ni muhimu sana kwasababu mchezo wa soka unapendwa sana Nigeria. Tulikuwa na presha nyuma yetu lakini tumejitahidi tumefanya kile tulichoweza kwa ajili yetu, familia zetu na Nigeria.”


ZeroDegree.
Nigeria yatwaa medali ya shaba kwenye mashindano ya Olympic. Nigeria yatwaa medali ya shaba kwenye mashindano ya Olympic. Reviewed by Zero Degree on 8/21/2016 11:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.