Loading...

Machinga Complex sasa ni kaa la moto.

Taswira ya Machinga Complex ikionekana kutoka juu:
MRADI wa jengo la Machinga Complex kwa ajili ya kutumiwa na wafanyabiashara ndogo ndogo jijini Dar es Salaam sasa ni kama kaa la moto linaloweza kuwachoma wale wote walio husika katika kuibua utata unaojitokeza kuhusiana na fedha zilizowekezwa.


Hali hiyo inatokana na taarifa kuwa sasa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imejitosa rasmi katika kuchunguza kwa kina juu ya kila kilichotokea katika sakata hilo linalohusisha tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya fedha na mwishowe kuwaburuza mahakamani wale wote watakao bainika kukiuka sheria za nchi.

Kuanza kwa uchunguzi huo wa Takukuru katika mradi wa Machinga Complex kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali uliofanywa na timu maalumu iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na ripoti yake kuonyesha kuwa kuna maswali mengi yaliyokosa majibu ya kujitosheleza na badala yake kuashiria uwapo wa rushwa na ufisadi ulionufaisha baadhi ya watu.

Mradi wa Machinga Complex ulitekelezwa kwa pamoja kutokana na mkataba ulioingiwa baina ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma za ufisadi katika mradi wa Machinga Complex, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Takukuru, Mussa Misalaba, alisema taasisi yao tayari imeanza kazi ya uchunguzi kuhusiana na tuhuma zilizopo zikiwamo za rushwa.

“Ni kweli tunaendelea na uchunguzi wa tuhuma za rushwa kuhusiana na ujenzi wa jengo hilo… tukikamilisha kila kitu kitawekwa hadharani. Lakini ndiyo, uchunguzi unaendelea kwa sasa,” alisema.

UTATA WENYEWE

Miongoni mwa madudu yaliyoibuliwa katika ripoti ya timu maalumu ya Makonda kuhusiana na Machinga Complex ni kwamba katika mkataba huo, jengo hali kujengwa kwa ukubwa uliotakiwa wa ghorofa sita bali ghorofa nne.

Aidha, uchunguzi huo wa timu ya Makonda iliyohusisha wataalamu mbalimbali ulibaini kuwa jengo hilo lina vizimba 4,200 badala ya 10,000 vilivyopaswa kujengwa kwa mujibu wa mkataba na zaidi ya hayo, vyumba hivyo vilijengwa kwa idadi hiyo pungufu kwa gharama ile ile iliyowekwa.

Jambo jingine lililoibua maswali ni kukabidhiwa kwa jengo hilo likiwa na deni la Sh. bilion19.7 lakini hadi kufikia Machi mwaka huu, deni hilo hilo limepanda hadi kufikia Sh. bilion 38 huku kiwango cha mkopo wa awali kikiwa ni Sh.bilion 12.7.
Wakati akitolea ufafanuzi kuhusiana na ripoti ya jengo hilo, Makonda alisema wamebaini jengo hilo halikujengwa kwa ukubwa sawa na ule ambao Halmashauri ya Jiji na NSSF walikubaliana kwenye mkataba ulioridhiwa na pande zote.

Aidha, Makondaalisemasuala la urejeshaji wa mkopo huo linazua utata mwingine mkubwa kwa sababu mkataba unaainisha kwamba mkopajia taanza kulipa marejesho ya deni kuanzia Desemba 31, 2008, muda ambao jengo hilo lilikuwa bado hata kukamilishwa na NSSF.

“Mkataba huu ni waovyo,haukupaswa kusainiwa. Inaonyesha kulikuwa na rushwa kwa pande zote mbili kwenye mkataba huu kwa sababu haiwezekani watu wana taaluma zao washindwe kuona udhaifu kwenye mkataba wa aina hii,” alisema Makonda.

Makonda alisema riba hiyo iliwekwa kiujanjaujanja na ndiyo sababu deni hilo limekuwa kubwa.

Alisema mkataba huo hauna tija kwa pande zote kwa sababu hautekelezeki na hauna faida kwa wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) ambao wameshindwa kuchukua vizimba kwa sababu gharama ya kupanga ni kubwa.

Aidha, Makonda alisema wamependekeza kuvunjwa kwa mkataba na NSSF kuchukua eneo lao kwamakubaliano kwamba Halmashauri ya Jiji italipwa kodi ya ardhi ya ketu.

“Pendekezo lingine ni kwamba NSSF wakabidhi jengo kwa Halmashauri ya Jiji lakini wakae na kukubaliana upya kwa kuandika mkataba tofautiana na ule waawali,” alisema Makonda, huku akisisitiza kuwa wahusika wote kutoka pande mbili za mkataba waliofanikisha mradi huo wachukuliwe hatua kwa sababu wametumia fedha za NSSF ambazo ni zawanyonge kwa faida ya watu wachache walio tanguliza maslahi binafsi.

Hivi karibuni Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) iliwasimamishakazi wakurugenzi sita, mameneja watano na mhandisi mmoja washirika hilo ilikupisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma kadhaa zikiwamo za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na taratibu katika uwekezaji, usimamizi wa miradi, manunuzi ya ardhi na ajira.

Taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, ilisema kwamba uamuzi huo umefanywa na Bodi chini ya mwenyekiti wake, Prof. Samwel Wangwe,iliyokutana Julai 15, mwaka huu kutokana na taarifa mbalimbali za wakaguzi wahesabu na shughuliza uendeshaji washirika hilo la umma.

Source: Nipashe
ZeroDegree.
Machinga Complex sasa ni kaa la moto. Machinga Complex sasa ni kaa la moto. Reviewed by Zero Degree on 8/21/2016 11:37:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.