Loading...

Okwi kutua tena Msimbazi..??


Straika Emmanuel Okwi.

SIKU chache baada ya wanachama wa Simba kuridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa timu huku mfanyabiashara, Mohammed Dewji, akitoa fedha kwa ajili ya usajili, jina la mshambuliaji wao kipenzi, Emmanuel Okwi, limetua ndani ya nyumba hiyo kwa ajili ya usajili.
Hivi karibuni uongozi wa Simba ulimwomba msaada bilionea huyo kuwapa fedha za usajili ili waweze kusajili wachezaji wazuri watakaoifanyia mambo makubwa timu hiyo na hivyo kutoa milioni 100.

Baada ya fedha hizo kumleta Mavugo, mashabiki na baadhi ya viongozi wamewasilisha jina la Okwi na tayari tangu juzi fununu kibao juu ya ujio wa mchezaji huyo zilienea katika mitandao ya kijamii kuhusu ujio wake.

Picha ambazo zilizagaa juzi kwenye mitandao ya kijamii zilizomwonyesha Okwi akiwa ndani ya ndege pamoja na kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kusababisha mjadala mkubwa huku ikidaiwa Mo amemleta mkali huyo wa kucheka na nyavu.

Mara baada ya kusambaa picha hizo kwenye mitandao ya kijamii hususani makundi ya Whatsap, wanadau wengi wa soka hususani wa Simba walionyesha ‘kuposti’ jumbe mbalimbali kuashiria kuwa bado wanamhitaji na wanamkaribisha ndani ya Msimbazi.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alivokuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema 
kuwa hana taarifa na ujio wa Okwi kwani wanaohusika na suala la usajili ni Kamati ya Usijali.

“Sina taarifa kama amekuja nchini tena kwa ajili ya kuitumikia Simba, hata hivyo wahusika ni kamati ya usajili lakini iwapo kama ni kweli ni jambo zuri ukizingatia alikuwa na mchango mkubwa kwenye timu kipindi tupo naye,” alisema.

Inakumbukwa kuwa Okwi aliichezea Simba kwa mafanikio makubwa na baadaye kuuzwa katika Klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia kisha kurejea Tanzania na kuitumikia Yanga.

Okwi alidumu kwa msimu mmoja tu Yanga ambayo aliingia nayo mgogoro na hivyo kurejea katika kikosi cha Simba kabla ya kujiunga na klabu ya Sonder-Jyske ya Denmark.


Credits: Bingwa
ZeroDegree.
Okwi kutua tena Msimbazi..?? Okwi kutua tena Msimbazi..?? Reviewed by Zero Degree on 8/08/2016 06:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.