Loading...

Rais Magufuli atoa zawadi ya Bajaji mlemavu anayejituma.

Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi funguo na nyaraka Bw. Thomas Kone (35) kwa ajili ya Bajaji mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumuona katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili.
 
Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi.

Bw. Thomas Kone akipanda kwenye bajaji aliyokabidhiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akisalimiana na Bw. Thomas Kone alipokwenda Kumkabidhi Bajaji kwa Niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Credits: Global Publishers
ZeroDegree.
Rais Magufuli atoa zawadi ya Bajaji mlemavu anayejituma. Rais Magufuli atoa zawadi ya Bajaji mlemavu anayejituma. Reviewed by Zero Degree on 8/19/2016 09:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.