Loading...

Rais Magufuli ateua Katibu mkuu mpya Wizara ya Fedha na Mipango.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Agosti,2016 amemteua Bw.Doto M.James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kabla ya uteuzi huo Bw.Doto M.James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

Bw.Doto M.James ataapishwa kesho tarehe 01 Septemba, 2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine.

Source: Local news [ ITV ]
ZeroDegree.
Rais Magufuli ateua Katibu mkuu mpya Wizara ya Fedha na Mipango. Rais Magufuli ateua Katibu mkuu mpya Wizara ya Fedha na Mipango. Reviewed by Zero Degree on 8/31/2016 08:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.