Loading...

Sepp Blatter mahakamani tena.

ALIYEKUWA Raisi wa zamani wa FIFA, Sepp Blatter anahudhuria mahakamani kusikiliza kesi inayoendeshwa na mahakama ya usuluhishi wa mizozo katika michezo nchini Uswizi.
Rais wa zamani wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA Sepp Blatter, anawasilisha rufaa yake ya mwisho mahakamahi hii leo dhidi ya marufuku aliyowekewa ya michezo na michezo kwa kukiuka madili.

Bw Blatter anahudhuria mahakamani kusikiliza kesi hiyo inayoendeshwa na mahakama ya usuluhishi wa mizozo michezoni nchini Uswizi.

Akizungumza na maripota mjini Lausanne, amejielezea kama mtu mwenye matumaini.

Bw Blatter aliwekewa marufuku hiyo mwezi Disemba mwaka jana kwasababu aliidhinisha malipo ya zaidi ya dola milioni mbili kwa mkuu wa zamani wa soka barani Ulaya , Michel Platini, miaka mitano iliyopita.

Mwezi Mei, Bw Platini alishindwa kushawishi kuondolewa kwa marufuku dhidi yake, ingawa ilipunguzwa kutoka miaka sita hadi miaka minne.

Credits: BBC Swahili
ZeroDegree.
Sepp Blatter mahakamani tena. Sepp Blatter mahakamani tena. Reviewed by Zero Degree on 8/26/2016 09:39:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.