Loading...

FBI ‘wamng’ang’ania’ Clinton.

Mgombea urais kupitia Chama cha Democratic, Hillary Clinton.
Nyaraka za Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) kuhusu uchunguzi unaomhusu mgombea urais kupitia Chama cha Democratic, Hillary Clinton, zinapitiwa upya kwenye jengo la Bunge la nchi hiyo.

FBI walikabidhi majalada yenye nyaraka hizo na ndani yake kuna barua kadhaa ambazo zinadaiwa kuandikwa na Clinton, akitumia anuani yake binafsi ya baruapepe, wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Wabunge wa Republican waliomba kupatiwa majalada hayo, baada ya FBI kusema kuwa hawana sababu ya kumfungulia mashtaka ya kukiuka itifaki ya mawasiliano, mgombea huyo urais anayewania kumrithi Rais Barack Obama.


ZeroDegree.
FBI ‘wamng’ang’ania’ Clinton. FBI ‘wamng’ang’ania’ Clinton. Reviewed by Zero Degree on 8/20/2016 08:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.