Loading...

Ugomvi wa laptop wasababisha kifo cha askari Jijini Mwanza.

Askari kwa kitengo cha upelelezi na makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza, G.5092 Pc John Nyanga, ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni katika eneo la villa pack club na mtu aliyekuwa na ugomvi naye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilitokea Agosti 21 mwaka huu, Saa 10:00 usiku na na kumtaja aliyefanya mauaji hayo kuwa ni Magina Selemani (27) mkazi wa kigoto wilayani Ilemela ambaye alikuwa fundi wa computer.

Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Ugomvi wa laptop wasababisha kifo cha askari Jijini Mwanza. Ugomvi wa laptop wasababisha kifo cha askari Jijini Mwanza. Reviewed by Zero Degree on 8/22/2016 10:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.