Loading...

VIDEO: Man City, Totenham na Chelsea zasonga, ...Liverpool yatandikwa bao mbili na Burnley bila kujitetea.

Man City wamefanikiwa kusonga mbele baada ya kupata ushindi wa goli 4 kwa 1 dhidi ya stoke city, magoli yakifungwa na Sergio Aguero(Goli 2) na Nolito(Goli 2). Kwa ushindi huo Man City inashikilia nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.



Msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza hadi hivi sasa:


Liverpool
ilishinda mechi yao ya kwanza kwa kuifunga 
 Arsenal goli 4 - 3, lakini leo imeshindwa kufua dafu kwa Burnley baada ya kufungwa goli 2 bila, huo ni ushindi wa nguvu kwa Burnley baada ya kurudi ligi kuu.

Burnley waliweza kutatua mitego yote ya Liverpool na kufanikwa kuongoza mchezo baada ya dakika mbili tu za mchezo kuanza. Nathaniel Clyne ndiye aliyetoa pasi ya mbali na Andre Gray kuingunisha kwa Sam Vokes ambaye aliutupia mpira nyavuni.

Dakika nane kabla ya mapumziko, Burnley wajihakikishia ushindi Baada ya kutupia bao la pili kwa counter-attack matata
. Ambapo Steven Defour alianzisha mpira wa mbali kwa Ragnar Klavan naye akauunganisha kwa Gray, ambaye aliucheza mara moja tu kabla ya kutupia nyavuni kwa kutumia mguu wake wa kushoto.

Kwa upande mwingine, Chelsea ilionekana kuduwaa muda mwingi uwanjani na kuja kupata ushindi katika dakika 10 za mwisho, lakini kwa mara ya pili mfululizo Diego Costa anafanikiwa kukwepa kadi nyekundu na kuifungia timu yake na kuipa ushindi wa goli 2-1.

Costa kwa mara nyingine tena anaonekana mwenye bahati ya kukwepa kadi nyekundu kwa ajili ya kadi mbili za njano. Wakati wa kipindi kipindi cha kwanza, yeye alionekana kujiangusha wazi katika eneo la penati lakini mwamuzi Jon Moss aliamua kutomchukulia hatua yoyote.


Victor Wanyama ndiye aliyefunga bao la pekee kwa kichwa lililowapa ushindi Tottenham dhidi ya Crystal Palace.


Leicester City na Arsenal wametoka sare ya bila kufungana kwenye uwanja wa King Power.

Wote(Arsenal na Leicester) wanabaki nyuma kwa pointi tano toka kwa Man City aliyekaa katika nafasi ya kwanza.

Arsenal walionekana kuwa timu bora lakini hawakuweza kupata bao. 
Leicester walikuwa na nafasi mbili ambazo zingewezakuwa penati kwao lakini mwamuzi Mark Clattenburg akazipotezea, ya kwanza ilikuwa pale Danny Drinkwater alipoangushwa katika sanduku la penati na Laurent Koscielny, na nyingine ilikuwa pale Hector Bellerin ilipogongana na Ahmed Musa.

Credits: ESPN 
ZeroDegree.
VIDEO: Man City, Totenham na Chelsea zasonga, ...Liverpool yatandikwa bao mbili na Burnley bila kujitetea. VIDEO: Man City, Totenham na Chelsea zasonga, ...Liverpool yatandikwa bao mbili na Burnley bila kujitetea. Reviewed by Zero Degree on 8/20/2016 10:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.