Loading...

Bilionea Moshi ajimwagia Petroli na kujipiga kiberiti.

MFANYABIASHARA maarufu na mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Merinyo, Manispaa ya Moshi, Roman Shirima (74), amejiua kwa kujimwagia mafuta ya petroli mwili mzima na kujilipua kwa kiberiti na kuteketea kwa moto.

Taarifa juu ya kifo hicho, zilithibitishwa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Wilbrod Mutafungwa.

Mfanyabiashara huyo alichukua uamuzi huo juzi saa 11:25 jioni nyumbani kwake eneo la Mjohoroni, Manispaa ya Moshi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa.
“Ni kweli tumepokea taarifa za mfanyabiashara huyo kujimwagia petroli na kujilipua kwa kiberiti na kisha kuteketea kwa moto hadi kufa, huko maeneo ya Mjohoroni, Manispaa ya Moshi. Chanzo cha yeye kufanya hivyo, bado hakijajulikana ila tunakichunguza,” alisema. 

Kabla ya kufikia uamuzi huo, inadaiwa asubuhi, alikwenda kusali na wanajumuiya wenzake wa Katoliki katika nyumba moja ya jirani.

Mabaki ya mwili wa mfanyabiashara huyo yalichukuliwa na polisi kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufani ya K.C.M.C kusubiri taratibu nyingine za kifamilia.

Ingawa, polisi wanasema baadhi ya wanafamilia waliitaarifu juu ya mfanyabiashara huyo kuonekana kujitenga mara kadhaa huku akiwa mpweke na aliyejawa na msongo wa mawazo, lakini kuna taarifa zisizo rasmi kutoka kwa baadhi ya watu wa karibu, kwamba awali alitaka kuuza shule hiyo.


Credits: Nipashe
ZeroDegree.
Bilionea Moshi ajimwagia Petroli na kujipiga kiberiti. Bilionea Moshi ajimwagia Petroli na kujipiga kiberiti. Reviewed by Zero Degree on 8/20/2016 10:33:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.