Loading...

VIDEO: Trump adai Obama na Clinton ndio waasisi wa kundi la kigaidi la IS.

MGOMBEA urais wa Chama cha Repuplican nchini Marekani, Donald Trump kwa mara nyingine ametoa kauli ya kuchefua baada ya kudai mpinzani wake Hillary Clinton na Rais Barack Obama waliasisi kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS).


Akiwahutubia wafuasi wake katika mji wa Fort Lauderdale, jimboni hapa juzi, bilionea huyo wa New York alisema ndiyo maana IS wamekuwa wakimtukuza Rais Obama.

Hayo ni matamshi ya karibuni zaidi tata kutoka kwa mgombea huyo, ambaye siku chache tu zilizopita, alitoa kauli iliyotafsiriwa na wengi kwamba zilichochea matumizi ya nguvu za bunduki dhidi ya Clinton, anayegombea urais kwa tiketi ya chama cha Democrat.




Katika matamshi yake ya Jumanne, Trump alionekana akidokeza kwamba Clinton anaweza kuuawa kwa kupigwa risasi kama njia ya kumzuia kuwateua majaji iwapo atashinda uchaguzi huo wa rais utakaofanyika Novemba 2016.


Credits: Mtanzania
ZeroDegree.
VIDEO: Trump adai Obama na Clinton ndio waasisi wa kundi la kigaidi la IS. VIDEO: Trump adai Obama na Clinton ndio waasisi wa kundi la kigaidi la IS. Reviewed by Zero Degree on 8/13/2016 07:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.