Loading...

Wachezaji wa kigeni Simba na Yanga kuitajirisha serikali.

WAKATI Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ikitarajiwa kuendelea kesho katika viwanja mbalimbali nchini, serikali inatarajia kuvuna kiasi cha Dola za Marekani 115,00 (zaidi ya Sh. milioni 240) kwa ajili ya ada za vibali vya wachezaji wa kigeni waliosajili katika klabu tatu kubwa.

Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa viongozi wa klabu za Simba, Yanga na Azam FC wako katika hatua za mwisho za kukamilisha malipo ya vibali vya wachezaji na makocha iliowaajiri. 

Imebainika kuwa ili mchezaji wa kigeni aweze kucheza soka hapa nchini atatakiwa kulipia kiasi cha Dola za Marekani 5,500 kwa ajili ya kulipia kibali cha kufanya kazi ambacho gharama yake ni Dola za Marekani 1,000 wakati ile inayokwenda uhamiaji ni Dola za Marekani 2,500.

Pia kila mchezaji anatakiwa kulipiwa ada inayokwenda katika mfuko maalumu wa maendeleo wa soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo ni Dola za Marekani 2,000.

Mbali na wachezaji, pia makocha wote wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini wanatakiwa kulipia kiasi cha Dola za Marekani 3,500 kwa mwaka.

'Kwa mfano sisi klabu yetu tunatakiwa kuwa na Sh. milioni 85 kwa ajili ya vibali hivyo," alisema mmoja wa viongozi wa klabu kongwe nchini.

Wachezaji wa Yanga ambao wanatakiwa kulipiwa ada hizo ni Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Obrey Chirwa kutoka Zimbabwe, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite (Rwanda), Vicent Bossou (Togo), Amissi Tambwe wa Burundi na Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm wa Uholanzi.

Kwa upande wa Simba wachezaji wanaotakiwa kulipiwa ni Laudit Mavugo wa Burundi, Juuko Murshid (Uganda), Method Mwajala (Zimbabwe), Frederick Blagnon, Vicent Angban (Ivory Coast), Mussa Ndusha na Janvier Bukungu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), makocha Joseph Omog (Cameroon) na Jackson Mayanja (Uganda).

Nyota wa Azam FC wanaohitaji kupata vibali ni Paschal Wawa, Michael Bolou (Ivory Coast), Jean Baptiste Mugiraneza (Rwanda), Racine Diof (Senegal), Daniel Amouh (Ghana) na Bruce Kangwa wa Zimbabwe pamoja na makocha wake wanaoongozwa na Mhispania Zeben Hernandes wanapaswa kulipiwa pia.

Credits: Nipashe
ZeroDegree.
Wachezaji wa kigeni Simba na Yanga kuitajirisha serikali. Wachezaji wa kigeni Simba na Yanga kuitajirisha serikali. Reviewed by Zero Degree on 8/26/2016 10:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.