Loading...

Walimu mbaroni kwa kunywa pombe saa za kazi.

Baadhi ya walimu wa shule ya msingi Chifunfu katika Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza wamekamatwa baada ya kukutwa wakinywa pombe saa za kazi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chifunfu, Lucas Mashinji amesema walimu hao walikutwa baa Julai 29 saa 3.15 asubuhi, baada ya raia wema kutoa taarifa kwa diwani wa eneo hilo, Robert Madaha.

Mashinji amesema walimu hao wanashikiliwa ofisi ya kata wakisubuiri taratibu nyingine kufanyika.

Diwani Madaha alisema taarifa za walimu hao alizipata kutoka kwa wananchi kuwa walimu hao wapo baa hivyo alitoa maagizo wakamatwe.

ZeroDegree.
Walimu mbaroni kwa kunywa pombe saa za kazi. Walimu mbaroni kwa kunywa pombe saa za kazi. Reviewed by Zero Degree on 8/01/2016 09:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.