Loading...

Wanne wahukumiwa kwenda jela miaka 60 baada ya kukutwa na meno ya tembo.

MAHAK AMA ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imewahukumu watu wanne wakiwemo ndugu wawili kutumikia kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na vipande 25 ya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 46 vikiwa na thamani ya Sh 371,600,000.



Ndugu hao wawili ni Boniphace Hoza (40) na Elias Hoza (46) wote wakazi wa Kijiji cha Kalela wilayani Kasulu katika Mkoa wa Kigoma. Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Makazi Mfawidhi Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ambao haukitia shaka yoyote.

Akitoa hukumu hiyo, Ntengwa aliwahukumu mkazi wa Kijiji cha Ivungwe katika makazi ya wakimbizi ya Katumba wilayani Mpanda, Justine Baruti (39) na mkazi wa kijiji cha Kalela, Boniphace Hoza kutumikia kifungo cha miaka 25 kila mmoja.

Wakati watuhumiwa wengine, kaka wa Boniface, Elias Hoza na Credo Gervas (45) mkazi wa kijiji cha Ndurumo, Katumba wamehumiwa kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Mahakama hiyo ilimwachia huru mshitakiwa wa tano, Sadock Masamba baada ya upande wa mashitaka kushindwa kutoa ushahidi wa kumtia hatiani mshitakiwa huyo.

Upande wa mashitaka uliongozwa na Wakili wa Serikali wa Mkoa wa Katavi, Wakyo Simon uliita mashahidi 15 na washitakiwa walitetewa na Wakili Elias Kifunda na hawakuwa na mashahidi wowote.

Awali, Mwendesha Mashitaka, Mwanasheria wa Serikali Wakyo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Desemba 24, 2014 katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani katika Mtaa wa Mji Mwema, Manispaa ya Mpanda.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa washitakiwa hao wamepanga kusafirisha nyara hizo za serikali kutoka mjini Mpanda hadi mkoani Kigoma kwa basi la abiria la Adventure Connection.

Iliendelea kudaiwa kuwa kutokana taarifa hizo askari wa Tanapa na Polisi walifika kwenye eneo la tukio na kuwakamata washitakiwa wakiwa na vipande 46 vya meno ya tembo ndani ya basi hilo la abiria.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa wa kwanza, Baruti siku hiyo alikamatwa na vipande 18 vyenye uzito wa kilo 33 vyenye thamani ya Sh milioni 49.6 na mshitakiwa wa pili Boniphace alikamatwa na vipande saba vya uzito wa kilo 13 na thamani ya Sh milioni 124 wakiwa wamevipakia kwenye basi la Kampuni ya Adventure Connection.


ZeroDegree.
Wanne wahukumiwa kwenda jela miaka 60 baada ya kukutwa na meno ya tembo. Wanne wahukumiwa kwenda jela miaka 60 baada ya kukutwa na meno ya tembo. Reviewed by Zero Degree on 8/21/2016 10:51:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.