Loading...

Wataalamu wa anga wamtembelea aliyetengeneza helikopta.

Wananchi wakitazama helkopta iliyotengenezwa na Adam Kinyekile.

Mkazi wa Tunduma mkoani Songwe, Adam Kinyekile aliyetengeneza helikopta ametembelewa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Kinyekile, ambaye pia ni fundi magari alisema ujumbe wa maofisa wanne kutoka TCAA Makao Makuu walifika ofisini kwake kwa ajili kuikagua helikopta hiyo. 

Aliwataja watalaamu hao kuwa ni Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Uendeshaji wa Ndege, Kapteni Kintu Newa; Mkaguzi Mkuu wa Usalama wa Ndege, Majaliwa Burhan; Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ubora wa Ndege; Abdillahi Mfinanga na Meneja wa TCAA- Mbeya, Victor Carlson.

Mmoja wa maofisa hao, Burhan amethibitisha kumtembelea Kinyekile, lakini alikataa kuzungumzia zaidi kwa maelezo kwamba wao walitumwa siyo wasemaji.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa undani kwani maofisa waliotumwa walitarajiwa kupitia mkoani Arusha kikazi na wakirudi Dar es Salaam watampa ripoti.

ZeroDegree.
Wataalamu wa anga wamtembelea aliyetengeneza helikopta. Wataalamu wa anga wamtembelea aliyetengeneza helikopta. Reviewed by Zero Degree on 8/01/2016 11:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.