Loading...

Chama cha ACT wazalendo kufanya mkutano wa demokrasia wiki hii.

Katibu wa Itikadi Uenezi na Mawasiliano ACT, Ado Shaibu.
CHAMA cha ACT Wazalendo kimetangaza kufanya Mkutano Mkuu wa Demokrasia Septemba 24 mwaka huu na kuhusisha wanachama, wadau wa siasa na wananchi kujadili masuala mbalimbali ya nchi.

Chama hicho kimetangaza kufanya mkutano huo licha ya jeshi la polisi kupiga marufuku mikutano yote ya nje na ndani inayohusu masuala ya siasa kwa kile kilichoelezwa kuwa inaleta uchochezi.

Hata hivyo, hivi karibuni, chama hicho kiliruhusiwa na Jeshi la Polisi kufanya kikao cha kamati kuu kwa kile kilichoelezwa kwamba ilibainika mkutano huo haukuwa na dalili za uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi Uenezi na Mawasiliano, Ado Shaibu, alisema mkutano huo ni utekelezaji wa katiba ya chama na hautajali kuwapo makatazo aliyoyaita batili.

“Mkutano Mkuu wa Demokrasia upo kwa mujibu wa katiba yetu ambayo imesajiliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa hivyo tutatekeleza wajibu wetu wa katiba bila kujali makatazo batili,” alisema.

Credits: Mtanzania
ZeroDegree.
Chama cha ACT wazalendo kufanya mkutano wa demokrasia wiki hii. Chama cha ACT wazalendo kufanya mkutano wa demokrasia wiki hii. Reviewed by Zero Degree on 9/19/2016 09:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.