Dirisha la usajili limefungwa, ..Luiz rasmi Chelsea, Nasri Sevilla, Mario Baloteli naye apata timu mpya.
Vilabu vya soka barani ulaya vimefanya usajili wa kumarisha vikosi vyao katika siku ya mwisho ya usajili uliofungwa usiku wa kuamkia Septemba mosi.
Inaarifiwa kuwa tayari Luiz amefuzu vipimo vya afya na kusaini mkataba ambao hata hivyo bado haujawekwa wazi.
PSG bado hawajasajili mbadala wa Luiz kutokana kuwa tayari na mabeki watatu wanaoweza kucheza katikati ambao ni Thiago Silva, Marquinhos na Presnel Kimpembe, huku Serge Aurier ambaye anacheza beki ya kulia akiwa pia na uwezo wa kufanya hivyo pia.
Moussa Sissoko amesajiliwa na Tottenham akitokea Newcastle kwa pauni milioni 30, Leicester City wamesajili Islam Slimani toka Sporting Lisbon kwa pauni milioni 29.
Stoke City wamemsajili Wilfried Bony kwa mkopo toka Manchester City, Samir Nasri nae amepelekwa kwa mkopo Sevilla toka kwa matajiri wa Man City.
Awali iliripotiwa kwamba, Nasri angejiunga na miamba ya Uturuki Besiktas, lakini mwishoni kabisa Sevilla wameonekana kuwa na mkono mrefu zaidi.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Sevilla Monchi ametanabaisha kwamba, Nasri ni mchezaji ambaye wamekuwa wakimfukuzia kwa muda wote kwenye dirisha hili la usajili.
Mkataba huo wa mkopo hauna kipengelea cha Nasri kununuliwa moja kwa moja endapo Sevilla watahitaji kufanya hivyo.
Valencia ya Hispania wamesamjili kwa mkopo wa muda mrefu Eliaquim Mangala wa Manchester City, Nao Juventus wamemsajili Juan Cuadrado kwa mkopo toka Chelsea kwa mkataba wa miaka mitatu.
Jack Wilshere ametua Bournemouth kwa mkopo wa msimu mzima, Mshambuliaji Mkongo Dieumerci Mbokani asajiliwa na Hull City. Enner Valencia aenda Everton kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka West Ham.
Chelsea wamemrejesha beki wao kisiki David Luiz waliomuuza miaka miwili iliyopita kwa Paris St- Germain, mchezaji huyu kanunuliwa kwa kiasi cha paundi million 34.
David Luiz |
Luiz (29) anarejea Chelsea baada ya kuondoka klabuni hapo miaka miwili iliyopita baada ya kusajiliwa ba PSG kwa ada ya paundi mil 50.
Inaarifiwa kuwa tayari Luiz amefuzu vipimo vya afya na kusaini mkataba ambao hata hivyo bado haujawekwa wazi.
PSG bado hawajasajili mbadala wa Luiz kutokana kuwa tayari na mabeki watatu wanaoweza kucheza katikati ambao ni Thiago Silva, Marquinhos na Presnel Kimpembe, huku Serge Aurier ambaye anacheza beki ya kulia akiwa pia na uwezo wa kufanya hivyo pia.
Moussa Sissoko amesajiliwa na Tottenham akitokea Newcastle kwa pauni milioni 30, Leicester City wamesajili Islam Slimani toka Sporting Lisbon kwa pauni milioni 29.
Stoke City wamemsajili Wilfried Bony kwa mkopo toka Manchester City, Samir Nasri nae amepelekwa kwa mkopo Sevilla toka kwa matajiri wa Man City.
Samir Nasri |
Manchester City wamethibitisha kiungo mshambuliaji wao Samir Nasri kujiunga na Sevilla kwa mkopo wa msimu mzima.
Awali iliripotiwa kwamba, Nasri angejiunga na miamba ya Uturuki Besiktas, lakini mwishoni kabisa Sevilla wameonekana kuwa na mkono mrefu zaidi.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Sevilla Monchi ametanabaisha kwamba, Nasri ni mchezaji ambaye wamekuwa wakimfukuzia kwa muda wote kwenye dirisha hili la usajili.
Mkataba huo wa mkopo hauna kipengelea cha Nasri kununuliwa moja kwa moja endapo Sevilla watahitaji kufanya hivyo.
Mario Baloteli |
Mshambuliaji Mario Balotelli wa Liverpool amesajiliwa na Nice ya Ufaransa bure, West Ham wamsajili beki Alvaro Arbeloa toka Real Madrid,
Valencia ya Hispania wamesamjili kwa mkopo wa muda mrefu Eliaquim Mangala wa Manchester City, Nao Juventus wamemsajili Juan Cuadrado kwa mkopo toka Chelsea kwa mkataba wa miaka mitatu.
Jack Wilshere ametua Bournemouth kwa mkopo wa msimu mzima, Mshambuliaji Mkongo Dieumerci Mbokani asajiliwa na Hull City. Enner Valencia aenda Everton kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka West Ham.
ZeroDegree.
Dirisha la usajili limefungwa, ..Luiz rasmi Chelsea, Nasri Sevilla, Mario Baloteli naye apata timu mpya.
Reviewed by Zero Degree
on
9/01/2016 10:09:00 AM
Rating: