Loading...

Hili hapa TAMKO la Serikali juu ya AGIZO la kukubali Mapenzi ya jinsia moja.

Serikali imesema kuwa haitakubaliana na mapendekekezo yaliyotolewa na baraza la kimataifa la haki za binadamu ambayo yanaenda kinyume na katiba ya nchi hususani suala la Mapenzi ya jinsia moja.



Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju katika warsha ya kuangalia na kujadili mapendekezo yaliyotolewa na baraza hilo ambapo amesema kuwa katika mapendekezo yaliyotolewa 227 wao kama serikali waliweza kuyakubali mapendekezo 130 na waliweza kukataa 72 na 25 kuyaweka kando.

Amesema nchi 23 zimepongeza msimamo huo wa serikali ya Tanzania na kuongeza kuwa serikali inatambua kuwa wako baadhi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ila katiba ya nchi inapingana na vitendo hivyo vinavyoweza kuyaharibu maadili ya Taifa huku akivitaka vyombo vya habari kusimama kidete kwa kuandika habari zinazopinga mapenzi ya jinsia moja.


kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) Onesmo Olenangoro ameitaka serikali kutoa uhuru wa kupatikana kwa habari bila kuwawekea vikwazo wanahabari katika kuripoti masuala mbali mbali.

ZeroDegree.
Hili hapa TAMKO la Serikali juu ya AGIZO la kukubali Mapenzi ya jinsia moja. Hili hapa TAMKO la Serikali juu ya AGIZO la kukubali Mapenzi ya jinsia moja. Reviewed by Zero Degree on 9/30/2016 07:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.