Loading...

Matokeo ya Ligi Kuu ya Vodacom jana Septemba 7, ..Simba, Azam zachekelea wakati Yanga ikilazimishwa sare ya bila kufungana.

Mgoli ya Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo yameipa Simba pointi tatu dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Ruvu Shooting ambao ndio wamepoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Simba katika mechi tatu walizocheza, walianza kupata goli lililofungwa na Abulrahman Mussa dakika ya saba kipindi cha kwanza.

Ajibu aliisawazishia Simba goli hilo dakika nne baadaye na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana bao 1-1.

Mavugo aliifungia Simba bao la pili na la ushindi dakika ya 48 kipindi cha pili akimalizia pasi ya Ibrahim Ajib.

Mchezo mwingine uliochezwa jana ulikuwa kati ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Dar es Salaam Youg Africans dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

Yanga ambao wanalitarajia kukutana na upinzania mkubwa kutoka kwa Ndanda FC kutokana na rekodi ya mechi zao za nyuma, wamelazimishwa suluhu ya 0-0 baada ya Ndanda kufanikiwa kucheza mchezo wakulinda goli lao kwani kipindi cha pili walicheza nyuma zaidi.

Mchezo huo unakuwa ni wa tano kwa Yanga na Ndanda FC kukutana katika Ligi Kuu sokaTanzania bara, lakini ni mara ya pili kwa timu hizo kucheza katika uwanja wa Nangwandahuku Yanga akiwa kafungwa mara moja katika uwanja huo na kutoa suluhu mara moja, kwa ujumla Yanga na Ndanda wamefungana mara moja moja na kutoka sare mara tatu.

Matokeo ya mechi nyingine ya Ligi kuu ya Vodacom iliyochezwa jana Septemba 7:

  • Tanzania Prisons 0 - 1 Azam FCGoli lilipatikana Kipindi cha pili dakika ya 59 kupitia kwa kiungo wa timu hiyo, Kipre Bolou.

ZeroDegree.
Matokeo ya Ligi Kuu ya Vodacom jana Septemba 7, ..Simba, Azam zachekelea wakati Yanga ikilazimishwa sare ya bila kufungana. Matokeo ya Ligi Kuu ya Vodacom jana Septemba 7, ..Simba, Azam zachekelea wakati Yanga ikilazimishwa sare ya bila kufungana. Reviewed by Zero Degree on 9/08/2016 09:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.