Loading...

FIFA yagomea rufaa ya Real na Atletico Madrid, ..imezifungia timu hizo kufanya usajili hadi January 2018.

Shirikisho la soka Ulimwenguni, FIFA limekataa rufaa ya Real Madrid na Atletico Madrid dhidi ya adhabu ya kuzifungiwa kufanya uhamisho wa wachezaji kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kukiuka maadili yaliyowekwa na shirikisho hilo.


FIFA inasema kuwa kamati yake ya rufaa imetupilia mbali rufaa ya klabu hizo mbili baada ya kubainika kwa vikwazo vya usajili mwezi Januari.

FIFA ilisema  kuwa, siku ya Alhamisi klabu hizo mbili tokea mji wa Madrid zilifungiwa kufanya usajili wa wachezaji wapya katika kipindi cha madirisha mawili ya uhamisho, hadi kufikia Januari 2018.

Ikumbukwe kuwa, klabu inaweza kufanya mikataba na kusainisha wachezaji lakini hawawezi kuwasajili na kuwatumia mashindandoni.

Klabu hizo mbili zinatarajiwa kukata rufaa kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo kujaribu kufutiwa adhabu hiyo.

"Kamati ya Rufaa ya FIFA imeamua kukataa rufaa iliyopelekwa na klabu hizo za Hispania, Atletico Madrid na Real Madrid na kuthibitisha ukamilifu wa maamuzi yanayotolewa na Kamati ya Nidhamu ya FIFA kuhusu kesi zinazohusiana na ulinzi wa wachezaji wenye umri mdogo(watoto)," FIFA ilisema.

"Kama ilivofahamika tangu awali, klabu zote hizo zinatakiwa kutumikia adhabu ya kutojihusisha na swala la uhamisho wa wachezaji katika ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa mfululizo wa vipindi/misimu miwili ya usajili baada ya kukiuka maadili ya makala namba 5, 9, 19 na 19bis na vile vile viambatisho namba 2 na 3 vya Kanuni za hadhi na usajili wa Wachezaji.

"Marufuku hiyo inazihusu klabu zote kwa ujumla - isipokuwa kwa upande wa timu za wanawake, futsal na 
timu za soka la mwambao(beach) - na vile vile haizuii timu hizo kuachana na wachezaji wake pale mikataba inapokuwa imefika mwisho.

"Zaidi ya hayo, Atletico Madrid na Real Madrid wamepigwa faini ya CHF 900,000 ambazo ni zaidi euro laki 8  na CHF 360,000 zaidi ya euro laki 3, na wakati huo klabu zote mbili zimepewa onyo na kutakiwa kulifanya rasmi na katika hali ya utaratibu uliopangwa na FIFA suala hilo la wachezaji wenye umri mdogo ndani ya siku 90."

Credits: ESPN Soccer
ZeroDegree.
FIFA yagomea rufaa ya Real na Atletico Madrid, ..imezifungia timu hizo kufanya usajili hadi January 2018. FIFA yagomea rufaa ya Real na Atletico Madrid, ..imezifungia timu hizo kufanya usajili hadi January 2018. Reviewed by Zero Degree on 9/08/2016 09:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.