Mo awamwagia noti wachezaji Simba.
SAA chache kabla mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba hapo kesho, mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji maarufu kama Mo ambaye hivi sasa ni mlezi wa klabu hiyo, amewajaza noti wachezaji wa timu hiyo na benchi zima la ufundi.
Taarifa ya Simba iliyotolewa jana na Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara, imeeleza kuwa Mo amelipa mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi kwa wakati hali ambayo imeongeza morali kuelekea katika pambano lao la kesho dhidi ya Yanga.
Mo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa barani Afrika, akiwa miongoni mwa matajiri vijana aliweka wazi miezi kadhaa iliyopita nia yake ya kumiliki hisa ya asilimia 51 ndani ya klabu hiyo.
Katika malipo hayo ya mishahara ya wachezaji, mfanyabiashara huyo amekuwa akitimiza jukumu lake hilo tangu Julai na hivi sasa uongozi wa timu hiyo unaamini kwamba suala hilo litatoa motisha mkubwa kwa timu hiyo kupata ushindi.
Katika hatua nyingine mfanyabiashara huyo pia anatarajia kulipa gharama za nyasi bandia za Uwanja wa Bunju na gharama nyingine za uendeshaji wa klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi.
Kuelekea katika mchezo wa kesho, Manara amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti ya kutosha timu yao iwezi kuibuka kidedea mbele ya watani zao Yanga.
“Naomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao, tunaamini mechi hiyo ni mwendelezo wa furaha kwa mashabiki na wanachama wetu wote nchini,” alisema Manara.

ZeroDegree.
Mo awamwagia noti wachezaji Simba.
Reviewed by Zero Degree
on
9/30/2016 10:26:00 AM
Rating: