Loading...

Matokeo ya Ligi ya Europa (VIDEO): Man U wafanikiwa kujiondoa mkiani mwa kundi, Genk ya Samatta yailaza Sassulo goli 3 kwa 1.

Ibrahimovic alifunga bao lake la sita tangu awasili United kutoka Paris St-Germain.
Manchester United wameondoka kwenye mkia kundi lao la ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, baada ya kupata ushindi dhidi ya Zorya Luhansk.

Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la pekee dakika ya 69, baada ya kombora la nguvu kutoka kwa Wayne Rooney kugonga mlingoti wa goli.

Hilo ndilo bao la kwanza la Ibra katika mechi tano, na lilitokana na kombora la kwanza la United lililolenga goli kwenye mechi hiyo.

United walitawala pakubwa mchezo huo uliochezewa Old Trafford, ingawa Sergio Romero alihitajika kufanya kazi ya ziada kuzima kombora la Paulinho muda mfupi kabla ya Ibrahimovic kufunga.

Mashetani hao Wekundu walitarajiwa kufanya vyema Europa League lakini walianza kampeni yao kwa kulazwa 1-0 na klabu ya Feyenoord ya Uholanzi mechi yao ya kwanza.

United sasa wamo nambari tatu kundini, wakiwa na alama sawa na Feyenoord na moja nyuma ya viongozi Fenerbahce wa uturuki ambao watazuru Old Trafford 20 Oktoba.

Rooney aanahitaji bao moja kufikia rekodi ya Ruud van Nistlerooy ya kufungia klabu hiyo mabao 38 michuano ya Ulaya.

United watarejea uwanjani Jumapili katika Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Stoke City dimba la Old Trafford.



Genk ikiwa nyumbani ilifanikiwa kuilaza Sassuolo ya Italia, bao tatu kwa moja ikiwa ni mchezo wa wa pili katika ligi ya Europa. Katika mchezo wao wa kwanza walifungwa na Athletic Bilbao ya Hispania, hivyo kufanya mchezo wao wa jana kuwa wa muhimu sana, nao kutochezea nafasi kwa yao ya pekee wakiwa uwanja wa nyumbani na kuondoka na pointi 3 muhimu.



Matoke yote ya mechi za Ligi ya Europa zilizochezwa jana ni kama ifuatavyo:




ZeroDegree.
Matokeo ya Ligi ya Europa (VIDEO): Man U wafanikiwa kujiondoa mkiani mwa kundi, Genk ya Samatta yailaza Sassulo goli 3 kwa 1. Matokeo ya Ligi ya Europa (VIDEO): Man U wafanikiwa kujiondoa mkiani mwa kundi, Genk ya Samatta yailaza Sassulo goli 3 kwa 1. Reviewed by Zero Degree on 9/30/2016 10:52:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.