Loading...

Rais Magufuli aahirisha ziara yake nchini Zambia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameahirisha zaira ya siku tatu nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa sita wa Jamhuri ya Muungano Zambia Mh.Edgar Chagwa Lungu.

Ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko la Ardhi lililosababisha vifo vya watu 16, mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera, Rais John Magufuli ameamua kuahirisha ziara yake hiyo.

Kufuatia kuahirisha ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumwakilisha katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu.

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe.Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika tarehe 13, September 2016 katika jiji la Lusaka.

ZeroDegree. 
Rais Magufuli aahirisha ziara yake nchini Zambia. Rais Magufuli aahirisha ziara yake nchini Zambia. Reviewed by Zero Degree on 9/11/2016 11:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.