Loading...

Rais Magufuli kushiriki sherehe za kuapishwa kwa rais wa Zambia.

Rais John Magufuli anatarajiwa kuwasili kesho Lusaka , Zambia kwa ziara ya siku tatu. Pamoja na mambo mengine atahudhuria pia sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia, Edgar Lungu zitakazofanyika kesho kutwa katika jiji la Lusaka.

Taarifa ya Mkurungenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa iliyotolewa leo inasema Rais Magufuli anafanya ziara hiyo ya kwanza nchini humo akiwa pia ni Mwenyekiti wa kamati ya siasa, ulinzi na usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).


Katika ziara hiyo Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika watakaohudhuria sherehe hizo.

ZeroDegree.
Rais Magufuli kushiriki sherehe za kuapishwa kwa rais wa Zambia. Rais Magufuli kushiriki sherehe za kuapishwa kwa rais wa Zambia. Reviewed by Zero Degree on 9/11/2016 06:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.