VIDEO: Mourinho ajutia juu ya uteuzi wa wachezaji alioufanya jana Man U ilipotandikwa na City goli 2 kwa 1.
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amekiri kuwa alikuwa na uwezo wa kupanga kikosi kingine mbali na kile alichochagua jana wakati timu yake ikikubali kipigo cha goli 2-1 nyumbani toka kwa mahasimu wao Manchester City.
Akiongea na Sky Sports, Mourinho alisema kuwa: "Kusema kweli, nilikuwa na wachezaji wangu wawili au watatu ambao niliwaanzisha kipindi cha kwanza ambapo, kama ningeijua kile ninachojua sasa, sidhani kama ningewaanzisha. Lakini hii ni kawaida ya soka, wakati mwingine wachezaji huwaangusha na kuwakatisha tamaa makocha na wakati mwingine hutoa mshangao mkubwa.
"Hawakunionyesha kile nilichotaka. Ni makosa yao na vile vile ni makosa yangu kwa sababu mimi ndiye meneja wao."
United ilikua nyuma kwa goli 2-0 kufuatia magoli ya Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho kabla ya Zlatan Ibrahimovic kuipatia goli la pekee timu yake muda mfupi tu kabla ya mapumziko, akitumia makosa ya kipa wa City, Claudio Bravo.
Katika majadiliano zaidi kuhusu mechi hiyo, Mourinho alisema kuwa: "Katika nusu ya kwanza, walikuwa bora zaidi kwani timu yangu ilianza mchezo vibaya kwani baadhi ya wachezaji walicheza chini ya kiwango cha kawaida..."
"Kipindi cha pili kilikuwa tofauti kabisa. Wakati wao walipofanya mabadiliko, na kumwingiza Fernando mapema, ni kwasababu walihisi tulitawala mchezo, ambapo ilikua ni hatari zaidi."
Katika mzungumzo zaidi, Mourinho aliongeza: "Mimi sikufanya mabadiliko baada ya dakika 20 kwa sababu sikutaka kuwaharibia mfumo wachezaji. Katika kipindi cha pili, tulibadili mwelekeo wa mchezo lakini hatukupata kile tulichostahili.."
"Hatukutawala mchezo [katika kipindi cha kwanza] na timu haikuwa ikiboresha mchezo - na ni vigumu kuboresha mchezo kwa maneno tu, kwa ujumla naweza sema Katika kipindi cha kwanza, tulifanya mambo mengi ovyo.."
Mourinho pia alisema kuwa baadhi ya wachezaji walishindwa kufuata maelekezo yake, ukiachana na beki Eric Bailly, ambaye mwenyewe alidai kuwa alikuwa makini na aliyehitaji matokeo mazuri hadi mwisho wa mchezo.
Kocha huyo alieleza: "..niliwaambia wakati wa mapumziko kwamba 'kwa baadhi yenu, inaonekana kama mnashindwa kufanya kile nilichowaelekeza kufanya.'...."
Awali Mourinho aliamua kumwanzisha Henrikh Mkhitaryan na Jesse Lingard kama wachezaji wa kati, wakati huo akimuacha nje Anthony Martial na Juan Mata. Mkhitaryan na Lingard walipumzishwa wakati wa mapumziko baada ya kushindwa kulimudu dimba vizuri, wakati huo Man City ilionekana kutawala zaidi.
Akiongea na Sky Sports, Mourinho alisema kuwa: "Kusema kweli, nilikuwa na wachezaji wangu wawili au watatu ambao niliwaanzisha kipindi cha kwanza ambapo, kama ningeijua kile ninachojua sasa, sidhani kama ningewaanzisha. Lakini hii ni kawaida ya soka, wakati mwingine wachezaji huwaangusha na kuwakatisha tamaa makocha na wakati mwingine hutoa mshangao mkubwa.
"Hawakunionyesha kile nilichotaka. Ni makosa yao na vile vile ni makosa yangu kwa sababu mimi ndiye meneja wao."
United ilikua nyuma kwa goli 2-0 kufuatia magoli ya Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho kabla ya Zlatan Ibrahimovic kuipatia goli la pekee timu yake muda mfupi tu kabla ya mapumziko, akitumia makosa ya kipa wa City, Claudio Bravo.
Katika majadiliano zaidi kuhusu mechi hiyo, Mourinho alisema kuwa: "Katika nusu ya kwanza, walikuwa bora zaidi kwani timu yangu ilianza mchezo vibaya kwani baadhi ya wachezaji walicheza chini ya kiwango cha kawaida..."
"Kipindi cha pili kilikuwa tofauti kabisa. Wakati wao walipofanya mabadiliko, na kumwingiza Fernando mapema, ni kwasababu walihisi tulitawala mchezo, ambapo ilikua ni hatari zaidi."
Katika mzungumzo zaidi, Mourinho aliongeza: "Mimi sikufanya mabadiliko baada ya dakika 20 kwa sababu sikutaka kuwaharibia mfumo wachezaji. Katika kipindi cha pili, tulibadili mwelekeo wa mchezo lakini hatukupata kile tulichostahili.."
"Hatukutawala mchezo [katika kipindi cha kwanza] na timu haikuwa ikiboresha mchezo - na ni vigumu kuboresha mchezo kwa maneno tu, kwa ujumla naweza sema Katika kipindi cha kwanza, tulifanya mambo mengi ovyo.."
Mourinho pia alisema kuwa baadhi ya wachezaji walishindwa kufuata maelekezo yake, ukiachana na beki Eric Bailly, ambaye mwenyewe alidai kuwa alikuwa makini na aliyehitaji matokeo mazuri hadi mwisho wa mchezo.
Kocha huyo alieleza: "..niliwaambia wakati wa mapumziko kwamba 'kwa baadhi yenu, inaonekana kama mnashindwa kufanya kile nilichowaelekeza kufanya.'...."
Msikilize the special one akizungumza hapo chini:
ZeroDegree.
VIDEO: Mourinho ajutia juu ya uteuzi wa wachezaji alioufanya jana Man U ilipotandikwa na City goli 2 kwa 1.
Reviewed by Zero Degree
on
9/11/2016 07:49:00 PM
Rating: