Loading...

Simba wazama kambini mapema kujiweka sawa na mechi ya Azam.

Kikosi cha Simba.
WAKATI Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), likipeleka mchezo wa Ligi Kuu kati ya Azam dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, kikosi cha kocha Joseph Omog jana kiliingia kambini kujiandaa na mchezo huo.


Awali, TFF ilitoa taarifa mwanzoni mwa wiki hii kuusogeza mchezo huo mbele hadi Septemba 21, lakini baada ya vikao vya jioni ya siku hiyo waliamua mchezo huo uchezwe Jumamosi kama ilivyopangwa, lakini sasa utafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru badala ya Uwanja wa Taifa.


Kikosi cha Simba kimeingia kambini juzi maeneo ya Dege beach kujiandaa na mchezo huo muhimu.
Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alithibitisha kupokea taarifa ya mchezo huo kufanyika kwenye Uwanja wa Uhuru na timu kuingia kambini.


"Tumepata taarifa mchezo wetu utachezwa kama ulivyopangwa, tunaendelea na mazoezi ya maandalizi," alisema Manara.
Haji alisema kuwa wachezaji wote wapo katika hali nzuri.


Mchezo huo ulikuwa na mkanganyiko baada ya taarifa ya kutaka kusogezwa mbele kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa mwenyeji wa mechi ya vijana - Serengeti Boys na Congo Brazzavile.

Credits: Nipashe
ZeroDegree.
Simba wazama kambini mapema kujiweka sawa na mechi ya Azam. Simba wazama kambini mapema kujiweka sawa na mechi ya Azam. Reviewed by Zero Degree on 9/14/2016 10:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.