Loading...

VIDEO: Messi aongeza idadi yake ya Hat - Trick UEFA.

Lionel Messi amefunga hat-trick yake ya sita kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya wakati Barcelona ikiiadabisha Celtic kwa kipigo kizito ambacho hawajawahi kukipata kwenye mashindano ya Ulaya.

Star huyo wa Argentina alianza kupachika bao la kwanza mapema katika mechi hiyo ya Kundi C.

Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishuhudia penati yake ikiokolewa kabla ya Messi kupasia kamba mara ya pili.

Kipindi cha pili Naymar alifunga kwa mpira wa adhabu ndogo kisha Iniesta akafunga goli la nne Messi akapachika bao la tano na Suarez akafunga pia bao jingine.

Magoli 266, assists 128

Kwenye misimu yao miwili wakicheza pamoja kwenye uwanja wa Nou Camp, Messi, Neymar na Luis Suarez kwa pamoja wamefunga magoli 253 huku wakiwa wame-assists mara 120.

Namba hizo zinakua kwa kasi wakati huu wa msimu mpya, magoli 266 na assists 128 ambapo Messi ameshapata hat-trick, Neymar amefunga na kutoa assists tano.

Historia mpya yawekwa

Hicho kilikuwa ni kipigo kikubwa zaidi kwa Celtic katika mashindano ya Ulaya. Celtic walikuwa vibonde mbele ya Barca. Miamba hiyo ya Catalan wameshatoa kipigo kama hicho kwa vilabu vingi vya aina hiyo na hiyo ndiyo faraja pekee kwa Celtic.

Kabla ya mchezo kocha wa Celtic Brendan Rodgers alisema, wachezaji wenye majina makubwa wanatafuta nafasi licha ya wapinzani wao kutumia mbinu za kila aina kujaribu kuwazuia.




Credits: ShaffihDauda
ZeroDegree.
VIDEO: Messi aongeza idadi yake ya Hat - Trick UEFA. VIDEO: Messi aongeza idadi yake ya Hat - Trick UEFA. Reviewed by Zero Degree on 9/14/2016 10:54:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.