Loading...

Stars wapewa tuzo nchini Nigeria.

Gavana wa Jimbo la Akwa Ibom nchini Nigeria, Udom Emmanuel.
GAVANA wa Jimbo la Akwa Ibom nchini Nigeria, Udom Emmanuel amewazawadia Sh milioni 21.7 wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ na wale wa Nigeria Sh milioni 46 baada ya mchezo wa kimataifa uliochezwa Nigeria mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika mechi hiyo ya mwisho ya makundi kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika mwakani, Stars ililala kwa bao 1-0. Timu hizo zote hazijasonga mbele kwenye michuano hiyo ambayo fainali zake zimepangwa kufanyika Gabon.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema kuwa Taifa Stars ilirejea nchini usiku wa kuamkia jana na kukiri kupewa fedha hizo na Gavana Emmanuel katika chakula cha usiku alichowaandalia wachezaji wa timu zote mbili.

“Taifa Stars walipewa dola za Marekani 10,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 21.7 na wachezaji wa Nigeria walipewa Naira milioni 10 ambazo ni sawa na Sh milioni 46 za kitanzania,” alisema Lucas.

Pia Lucas alisema gavana huyo alitoa fedha hizo kutokana na ari ya upiganaji waliyoonesha wachezaji wa Taifa Stars wakiongozwa na nahodha Mbwana Samatta ambaye kabla ya mchezo huo alikuwa gumzo kwa Wanigeria. Tanzania haijawahi kuifunga Nigeria katika michezo yote waliyowahi kucheza nao zaidi ya kutoka sare.

Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Stars wapewa tuzo nchini Nigeria. Stars wapewa tuzo nchini Nigeria. Reviewed by Zero Degree on 9/06/2016 09:17:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.