Loading...

Yanga, Simba zapigana chenga kwa Kessy.

VIONGOZI wa Simba na Yanga wameonekana kupigana chenga juu ya kuhudhuria kikao cha Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa ajili ya kutoa hukumu ya shauri la beki, Hassan Kessy, baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho.

Mara kadhaa viongozi wa Simba na Yanga wameonekana kuwa na udhuru kila linapofika suala hilo kujadiliwa ambapo katika vikao vinne ilivyokaa kamati hiyo viongozi wa Yanga walihudhuria vikao vitatu huku wale wa Simba wakihudhuria kimoja.


Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, mara zote Yanga wamekuwa wakihudhuria vikao hivyo isipokuwa kimoja ambacho kilifanyika mwishoni wiki iliyopita ndio hawakuhudhuria kutokana na kuwa na dharura.

“Sisi tumehudhuria zaidi ya vikao vitatu, kimoja ndio tumekosa sasa hatujui nini hatima ya hili suala mpaka hapo baadaye watakapotuita tena kuwasikilize,” alisema Baraka.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, wiki iliyopita alisema kwamba kikao hicho kiliahirishwa kutokana na wajumbe wa kamati hiyo kuwa na udhuru hivyo kushindwa kufanyika.

Kessy anadaiwa na Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na klabu ya Yanga sambamba na kusajili katika timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani kabla ya mkataba wake kufika mwishoni Juni 15, 2016.

Simba iliwasilisha malalamiko mbele ya kamati hiyo ya TFF kwamba Kessy alivunja taratibu hizo akiwa ndani ya mkataba wa klabu hiyo yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Credits: Bingwa
ZeroDegree.
Yanga, Simba zapigana chenga kwa Kessy. Yanga, Simba zapigana chenga kwa Kessy. Reviewed by Zero Degree on 9/06/2016 10:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.