Loading...

VIDEO: Lukaku na Hat - Trick matata, ..magoli matatu ndani ya dakika 12.

Lukaku kafunga mabao matatu ndani ya dakika 12 za kipindi cha pili na kuipa Everton ushindi wagoli 3 - 0 dhidi ya Sunderland siku ya Jumatatu, mbele ya kocha wao wa zamani David Moyes ambaye kwa sasa yuko na klabu ya Sunderland.

Everton imepiga hatua na kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kwa kuwa na 10 kama Chelsea. Sunderland ni ya 19 katika msimamo wa ligi, ikiwa na point moja tu.


Idrissa Gueye na Yannick Bolasie ndio waliomng'arisha Lukaku kwa kumpa pasi zilizozaa magoli mawili yote akiyafunga kwa kichwa, kabla ya Mirallas kutoa pasi ya usaidizi(assist) kwa mbelgiji huyo naye bila makosa akatupia goli la tatu.


ZeroDegree.
VIDEO: Lukaku na Hat - Trick matata, ..magoli matatu ndani ya dakika 12. VIDEO: Lukaku na Hat - Trick matata, ..magoli matatu ndani ya dakika 12. Reviewed by Zero Degree on 9/13/2016 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.