Loading...

Wayne Rooney avunja rekodi Uingereza.

Rooney kavunja rekodi, kachukua nafasi ya David Beckham na kuwa mchezaji aliyeshiriki katika michezo mingi zaidi na timu yake ya taifa ya Uingereza.

Rooney mwenye umri wa miaka 30, alitimiza mechi yake ya 116 ya kimataifa siku ya Jumapili wakati Uingereza ikitafuta nafasi kushiriki Kombe la Dunia dhidi timu ya taifa ya Slovakia, ambapo pia ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Sam Allardyce kama kocha mpya wa Uingereza.

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce.
Mshambuliaji huyo amebakizwa kikosini kama nahodha wa kocha mpya wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce. Lakini kwa upande wa Rooney yeye anasema anampango wa kustaafu kutoka katika kibarua cha kuitumikia timu yake ya taifa baada ya  kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2018

Kwa wakati huo, Rooney atakua na  matumaini ya kuvunja rekodi ya Uingereza ya kuonekana mara 125 katika timu yake ya taifa, rekodi iliyowekwa na kipa Peter Shilton kati ya mwaka 1970 na 1990.

Rooney alionekana kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Uingereza mwaka 2003 akiwa na
 umri wa miaka 17. Ingawa amefanikiwa kushinda kila taji kubwa akiwa na klabu ya Manchester United, hatua kubwa ambayo Wayne Rooney amewahikufika katika mashindano makubwa akiwa na Uingereza ni hatua ya robo fainali ya mwaka 2004 katika michuano ya Ulaya(Euro 2004) na Kombe la Dunia mwaka 2006.

Credits: NBC Sports
ZeroDegree.
Wayne Rooney avunja rekodi Uingereza. Wayne Rooney avunja rekodi Uingereza. Reviewed by Zero Degree on 9/05/2016 11:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.