Loading...

Aliyekuwa Spika wa bunge la Brazil akamatwa kwa tuhuma za rushwa.

Amekuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa wenye nguvu kubwa kwa miaka mingi.
Spika wa zamani wa bunge la Brazil, Eduardo Cunha amekamatwa akihusishwa na rushwa.

Bwana Cunha alituhumiwa kwa kuchukuwa dola milioni tano kama hongo kutoka kwa kampuni ambayo ilishinda mikataba na kampuni ya mafuta ya serikali, Petrobras.

Amekuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa wenye nguvu kubwa kwa miaka mingi.

Aliongoza mashtaka dhidi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff, ambaye aliondolewa madarakani mwezi Agosti.

Eduardo Cunha alijiuzulu katika wadhifa wake mwezi Julai 2016.
Cunha aliondolewa kutoka bunge la Brazil mwezi uliopita kwa kudanganya kuhusu kuwa na mamilioni ya dola katika akaunti za benki nchini Switzerland.

Source: BBC Swahili
ZeroDegree.
Aliyekuwa Spika wa bunge la Brazil akamatwa kwa tuhuma za rushwa. Aliyekuwa Spika wa bunge la Brazil akamatwa kwa tuhuma za rushwa. Reviewed by Zero Degree on 10/20/2016 08:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.