Loading...

Chama cha wananchi [ CUF ] kimewafungulia mashtaka rasmi Jaji Mutungi na Prof. Lipumba.

Chama cha CUF kimefungua kesi dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na msajili huyo, Profesa Ibrahim Lipumba.

Kesi hiyo namba 23 ya 2016 ilifunguliwa jana na Bodi ya Wadhamini wa CUF Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya Mahakama hiyo kuridhia maombi ya chama hicho ya kibali cha kumfungulia kesi msajili.

Wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wananchi 11 waliosimamishwa uanachama na CUF, akiwamo Naibu Katibu Mkuu (Bara) ambaye pia ni mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya.

Bodi hiyo inaiomba Mahakama itoe amri kubatilisha barua ya Msajili inayomtambua Profesa Lipumba kuwa ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CUF.

ZeroDegree.
Chama cha wananchi [ CUF ] kimewafungulia mashtaka rasmi Jaji Mutungi na Prof. Lipumba. Chama cha wananchi [ CUF ] kimewafungulia mashtaka rasmi Jaji Mutungi na Prof. Lipumba. Reviewed by Zero Degree on 10/20/2016 08:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.