Loading...

Fifa kuongeza washiriki wa kombe la dunia, hadi kufikia timu 48.

Gianni Infantino.
Rais wa Fifa Gianni Infantino ameshauri kuongezwa kwa timu zinazoshiriki kombe la dunia na kufikia 48 zaidi ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiwania nafasi hiyo kuwa atafikisha timu 40.


Anashauri kuwa timu 16 kati ya zote zitatolewa katika hatua ya awali kabisa.

Kisha kubaki 32 zitakazoendelea katika makundi baada ya hatua ya mtoano kukamilika.

Infantino anasema kuwa mapendekezo hayo yatapelekwa katika bodi ya Fifa Januari.

''Haya ni mawazo ya kupata suluhisho la uhahika, tutayajadili mwezi huu na kufahamu nini cha kufanya mwaka 2017,'' alisema Infantino mwenye miaka 46.

Infantino aliingia madarakani kuliongoza shirikisho hilo la Fifa mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.


ZeroDegree.
Fifa kuongeza washiriki wa kombe la dunia, hadi kufikia timu 48. Fifa kuongeza washiriki wa kombe la dunia, hadi kufikia timu 48. Reviewed by Zero Degree on 10/04/2016 09:26:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.