Kamera kuwakamatisha waliofanya uharibifu wa viti Uwanja wa Taifa.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema litatumia picha za video katika kuwakamata mashabiki wanaodaiwa kuvunja viti katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, alisema jana kuwa jeshi hilo limesikitishwa na kitendo hicho hivyo kuahidi kuwafuatilia na kuwatia nguvuni wale wote waliohusika kufanya uharibifu wa mali za uwanja.
“Kamera zilizokuwepo uwanjani zimeonyesha tukio lilivyokuwa, hivyo tutatumia picha hizo katika kuwasaka na kuwatia nguvuni wote walioshiriki katika kung’oa viti,” alisema Kamanda Sirro.
Alisema changamoto iliyokuwepo uwanjani hapo ilikuwa ni kubwa japo askari walijitahidi kudhibiti kwa kutumia mbinu mbalimbali.
“Nitoe wito kwa mashabiki wa mpira kuhakikisha wastaarabu na kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Sirro.
Tukio hilo lilitokea wakati wa pambano baina ya Simba na Yanga lililofanyika Jumamosi iliyopita, ambapo mashabiki wanaodaiwa wa Simba walivunja viti wakionyesha hisia zao baada ya wapinzani wao kuandika bao la kuongoza kupitia mshambuliaji, Amissi Tambwe.
- Simba na Yanga wamepigwa marufuku kutumia uwanja wa Taifa.
- VIDEO: Jinsi Hamis Tambwe alivyounawa mpira kabla ya kuifungia Yanga goli.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, alisema jana kuwa jeshi hilo limesikitishwa na kitendo hicho hivyo kuahidi kuwafuatilia na kuwatia nguvuni wale wote waliohusika kufanya uharibifu wa mali za uwanja.
“Kamera zilizokuwepo uwanjani zimeonyesha tukio lilivyokuwa, hivyo tutatumia picha hizo katika kuwasaka na kuwatia nguvuni wote walioshiriki katika kung’oa viti,” alisema Kamanda Sirro.
Alisema changamoto iliyokuwepo uwanjani hapo ilikuwa ni kubwa japo askari walijitahidi kudhibiti kwa kutumia mbinu mbalimbali.
“Nitoe wito kwa mashabiki wa mpira kuhakikisha wastaarabu na kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Sirro.
ZeroDegree.
Kamera kuwakamatisha waliofanya uharibifu wa viti Uwanja wa Taifa.
Reviewed by Zero Degree
on
10/04/2016 09:41:00 AM
Rating: