Loading...

Kauli ya Mourinho kuhusu mwamuzi wa mechi ya Man U dhidi ya Liverpool kuchunguzwa na FA

Mourinho amesema itakuwa vigumu kwa mwamuzi huyo kuchezesha vizuri baada ya uteuzi wake kukosolewa.
Matamshi ya Jose Mourinho kuhusu uteuzi wa mwamuzi anaeshabikia Manchester United Anthony Taylor kwa mchezo wa ligi kuu England kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool utakaochezwa leo jumatatu yatachunguzwa na Shirikisho la Mpira wa miguu nchini humo FA.

Mourinho amesema itakuwa vigumu kwa mwam.uzi huyo kuchezesha vizuri baada ya uteuzi wake kukosolewa.

'Mtu mmoja akiwa na lengo anaweka shinikizo kwake' alisema Mourinho

Kwa kawaida makocha hawatakiwi kuzungumza lolote kuhusiana na mwamuzi kabla ya mchezo.


Anthony Taylor hajatoa kadi yoyote nyekundu msimu huu.
FA inataka kuchunguza matamshi hayo kabla ya kuamua ni hatua gani kama itapatikana, inaweza kuchukuliwa.

Uteuzi wa Taylor, umekosolewa na Kenith Hackett,mkuu wa Bodi ya marefarii Professional Game Match Officials Ltd.


ZeroDegree.
Kauli ya Mourinho kuhusu mwamuzi wa mechi ya Man U dhidi ya Liverpool kuchunguzwa na FA Kauli ya Mourinho kuhusu mwamuzi wa mechi ya Man U dhidi ya Liverpool kuchunguzwa na FA Reviewed by Zero Degree on 10/17/2016 03:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.