Loading...

Hizi hapa AGENDA za klabu ya Yanga kuelekea mkutano mkuu Octoba 23.

Yanga imetoa agenda ambazzo zitajadiliwa kwenye Mkutano Mkuu wa dharura unaotarajiwa kufanyika October 23, 2016.


Agenda inayosubiiwa kwa hamu ni agenda namba 11 ambapo Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji ataweka wazi msimamo wake juu ya maazimio ya wanachama kwenye kikao.



Ajenda za mkutano mkuu wa dharura wa wananchama Tarehe 23 Oktoba, 2016 kwenye uwanja kaunda.

1. Sala na Utambulisho wa wageni waalikwa:

1.1. Sala ya Wakristo ya Kubariki Kikao.

1.2. Sala ya Waislamu ya Kubariki Kikao.

1.3. Utambulisho wa wageni waalikwa waliohudhuria, pia wenye udhuru – Waziri wa Michezo na Sanaa; Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT), Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Dar-Es-Salaam (DRFA) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 2. Kufungua kikao.

3. Kupitia dondoo za kikao kilichopita cha mkutano wa wanachama na kuidhinisha.

4. Kuthibitisha wajumbe wa bodi ya wadhamini na kumpumzisha mjumbe mmoja na kuongeza mjumbe mwingine kwenye baraza la wadhamini.

Mwenyekiti kuomba ridhaa ya kumteua mjumbe mmoja bila ya kuitisha mkutano mkuu kupunguza gharama kwa klabu.

5. Kupitia na kujadili muhitasari wa majadiliano ya bodi ya wadhamini kulingana na maagizo ya wananchama kukodisha timu ya Yanga na nemba ya Yanga kwa kipindi cha miaka kumi/ na kupata maamuzi kupitia kura za wananchama.

6. Kujadili mwenyekiti abaki kama mwenyekiti au kulingana na maslahi yake kwenye kampuni, kama italeta mgongano katika kampuni yake inayokodisha timu ya Yanga na nembo ya Yanga kwa kipindi cha miaka kumi ili kupata maamuzi kupitia kura za Wanachama.

7. Kurudia kupitia marekebisho ya katiba iliyoagizwa na wanachama kupitia marekebisho ya katibabiliyoagizwa na wanachma kupitia vikao vyao mbalimbali na baadhi kukataliwa na TFF, baadhi hazijasajiliwa kazi na BMT na baadhi RITA wamezikalia bila kuzifanyia kazi kwa sababu zisizojulikana. Kupata msimamo wa wananchama kwa kuzingatia katiba ya Yanga inayosema mikutano ya wananchamandio yenye mamlaka ya mwisho ilimradi tu maamuzi hayo yaangukie ndani ya sheria za nchi na si sahihi vyombo hivyo kuingilia maamuzi halali ya wananchama.

8. Kupitia utendaji wa kamati ya mashindano, Ratiba ya ligi kuu bara, adhabu ya Yanga kutoka wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo ambayo ilisababishwa na fujo za mashabiki wa Simba.

9. Kupata maamuzi juu ya wananchama ambao hawafiki katika mikutano badala yake wanakuwa wasemaji wa Yanga bila kuwa na mamlaka hayo na kuleta uchonganishi wa wazi ndani ya klabu, kupotosha jamii na kuchafua majina ya viongozi wa klabu.

10. Tarehe ya ucaguzi mdogo kujazia nafasi zilizowazi na kupata mwongozo wakutumia katiba ipi kati ya 2010 au 2014. Pamoja na masahihisho baada ya 2014, au bila ya masahihisho ya 2014 yaliyoamliwa na wanachama.

11. Hotuba ya mwenyekiti – Maoni na msimamo wake wajuu ya maazimio ya wanachama kwenye kikao;

kusema anayoyajua ya siri kuhusu Yanga na adui wa Yanga na kufafanua wanaoleta vurugu Yanga, baadhi ni mamluki wa wafanyabiashara wenzake walioshindwa kumshinda kwa njia halali na sasa wanaitumia Yanga kama sehemu pekee iliyobakia kumuumiza kupitia mbinu zinazotumika hasa kwa kuleta vurugu ndani ya Yanga ili kumchafua yeye binafsi, kufanya kwao hivyo ni kushusha hadhi ya klabu na maoni yake kwa maslahi ya Yanga, kipi kifanyike.

12. Mengineyo.

13. Sala.

13.1. Sala ya Waislamu ya Kubariki Maamuzi ya Mkutano.

13.2. Sala ya Wakristo Kubariki Maamuzi ya Mkutano.

14. Kufunga mkutano.

ZeroDegree.
Hizi hapa AGENDA za klabu ya Yanga kuelekea mkutano mkuu Octoba 23. Hizi hapa AGENDA za klabu ya Yanga kuelekea mkutano mkuu Octoba 23. Reviewed by Zero Degree on 10/17/2016 05:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.