Loading...

Timbwili la Yanga kukodishwa.

Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga, Francis Kifukwe (kushoto) akiwa na yusuph manji (katikati).
BARAZA la Wadhamini la Klabu ya Yanga, limesema kabla ya kufikia uamuzi wa kuikodisha timu kwa Kampuni ya Yanga Yetu, liliomba msaada wa kisheria kutoka kwa magwiji wa taaluma hiyo nchini.
Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga, Francis Kifukwe aliliambia Nipashe jana kwamba, baada ya kuandaa muswada wa kukodisha timu kwa pamoja na wakodishwaji, waliupeleka kwa wanachama wao ambao ni magwiji wa sheria nchini kuomba msaada wa kisheria. 


Kifukwe amewataja magwiji hao kuwa ni Profesa Mgongo Fimbo, Jaji John Mkwawa na Alex Mgongolwa ambao wote waliafiki muswada huo na kuusifia, kwamba ni nafasi adimu klabu inapata.

“Baada ya kupata msaada huo wa mawazo ya kisheria kutoka kwa magwiji hao wa sheria, tukajiridhisha na kwa kuwa taratibu zilikwishafuatwa tukaafiki huo mpango na kuuupitisha,”alisema Kifukwe.

Kuhusu madai ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwamba Baraza la Wadhamini lililopitisha mpango huo halitambuliwi, Kifukwe alisema si kweli.

“Kwanza huyo mtu anayetajwa Juma Mwambelo, hajawahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga. Baada ya Baraza la Wadhamini wa zamani wa klabu wengi wao kufariki dunia, liliundwa baraza lingine na BMT ilishirikishwa, ambalo ndilo tumo ndani yake,”alisema.

Kifukwe, Rais wa zamani wa Yanga SC, aliwataja wanaounda baraza hilo mbali na yeye, wengine ni Kapteni Mstaafu George Mkuchika, Mama Fatuma Karume, Amri Ramadhan, Juma Kambi na Abeid Mohammed.

Na kuhusu madai ya baraza hilo kuikodisha timu ya soka kwa Yanga Yetu bila ridhaa ya BMT, Kifukwe alisema: “Maamuzi ya wanachama hayahitaji Baraka za BMT, sana kama kuna mapungufu wameyaona wauandikie uongozi kuuelekeza cha kufanya.”

Credits: Nipashe
ZeroDegree.
Timbwili la Yanga kukodishwa.  Timbwili la Yanga kukodishwa. Reviewed by Zero Degree on 10/09/2016 03:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.