Loading...

Majeruhi kumkosesha Juma Abdul mechi zote zilizosalia.

BEKI wa Yanga, Juma Abdul, atakosa mechi zote zilizosalia za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na kuwa majeruhi.

Yanga imesaliwa na mechi dhidi ya Mbao FC, Mbeya City na Tanzania Prisons kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.



Abdul aliumia katika mechi ya ligi hiyo dhidi ya Azam iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, iliyomalizika kwa sare tasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana daktari wa timu hiyo, Edward Samweli, alisema beki huyo ataendelea kukosa mechi kutokana na tatizo kuwa kubwa.

Samweli alisema kesho anatarajiwa kwenda kufanyiwa kipimo kikubwa ili apatiwe matibabu zaidi.

“Mchezaji huyu atakosekana katika michezo ijayo na kama hali yake haitabadilika huenda akarudi mzunguko wa pili wa ligi kuu,” alisema Samweli.

Tayari beki huyo amekosa mechi tatu dhidi ya Toto Africans, Kagera Sugar na JKT Ruvu iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

ZeroDegree.
Majeruhi kumkosesha Juma Abdul mechi zote zilizosalia. Majeruhi kumkosesha Juma Abdul mechi zote zilizosalia. Reviewed by Zero Degree on 10/28/2016 10:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.