Loading...

Watu 6 wafutiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Mahakama ya Rufani imewafutia adhabu ya kunyongwa hadi kufa na kuamuru kuachiwa huru watu sita waliohukumiwa kwa mauaji ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na mfanyakazi wa Benki ya NMB, tawi la Wami Morogoro.


Uamuzi huo ulisomwa jana na Jaji Projest Rugazia wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam baada ya kutolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani lililoongozwa na Jaji Mkuu, Mohamed Chande. Wengine ni Jaji Ibrahimu Juma na Jaji Augustine Mwarija.



Jopo hilo lilikubali hoja za warufani waliowakilishwa na mawakili Richard Rweyongeza, Majura Magafu, Barnabas Luguwa, Samson Mbamba na Gabinus Galikano kuwa Mahakama Kuu ilikosea kuwatia hatiani kwa kuwa haikuwa na ushahidi wa kutosha.


ZeroDegree.
Watu 6 wafutiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa. Watu 6 wafutiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa. Reviewed by Zero Degree on 10/28/2016 09:51:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.