Loading...

Mamelodi Sundowns yatwaa ubingwa wa Afrika 2016.

Licha ya kupoteza mchezo wao wa marudiano, Mamelodi Sundowns wametangazwa mabibwa wa Afrika kwa ngazi ya vilabu mwaka 2016 baada ya kuruhusu kufungwa ngoli 1-0 na wenyeji Zamalek ya Misri kwenye mji wa Alexandria siku ya Jumapili.

Matokeo hayo yanaifanya Sundowns kushinda kwa ya magoli 3-01 baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa magoli 3-0 huko Atteridgeville Afrika Kusini Jumamosi iliyopita.

Taji hilo ni la kwanza kwa klabu hiyo ya Afrika Kusini ambayo fainali yake ya mwisho katika michuano hiyo ilikuwa ni 2001 ambapo ilipoteza mbele ya Al Ahly ambao ni mahasimu wakubwa wa Zamalek.

Zamalek walipata goli lao la pekee dakika ya 62 kutoka kwa Stanley Ohawuchi licha ya kutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa.

Ubora wa safu ya ulinzi ya Sundowns uliwafanya waweze kulinda ushindi wao walioupata nyumbani kwenye mchezo wa kwanza.

Baada ya kusema mashabiki 20,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia pambano hilo kwa sababu za kiusalama, mamlaka ya Misri waliruhusu mashabiki 86,000 kuingia uwanjani kushuhudia mtanange huo ili kutoa support kwa timu yao.

ZeroDegree.
Mamelodi Sundowns yatwaa ubingwa wa Afrika 2016. Mamelodi Sundowns yatwaa ubingwa wa Afrika 2016. Reviewed by Zero Degree on 10/24/2016 09:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.