Mwinjilisti 'Komando Wa Yesu' aja na mpya, ..aiomba serikali kufuta msamaha wa kodi kwa taasisi za kidini.
Mwinjilisti Daudi Mashimo wa Kanisa la Carvary Mision. |
Mwinjilisti wa Kanisa la Carvary Mision ameiomba Serikali kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi zote za kidini akidai misamaha hiyo haina manufaa kwa wananchi wala taifa bali kwa taasisi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwinjilisti Daudi Mashimo amesema licha ya misamaha ya kodi, taasisi hutoa huduma kwa gharama kubwa ilihali hazilipi kodi.
"Ukimpeleka mwanao shule za dini ni aghali sana na hata hospitali za misheni ni aghali pia sasa watu hawa wana manufaa gani kwa jamii na taifa maana kodi hawalipi wala huduma zao hazina unafuu kwa wananchi," amesema.
Ameongeza kuwa taasisi kutolipa kodi ni kosa kwani kodi ndio inaendesha nchi na kuleta maendeleo na taasisi za dini zilipaswa kuwa kiongozi.
"Yesu mwenyewe alikuwa akilipa kodi na alikuwa anajenga nchi yake, wao wanaomba tu kufutiwa kodi na hawatumii msamaha ipasavyo," ameongeza.

ZeroDegree.
Mwinjilisti 'Komando Wa Yesu' aja na mpya, ..aiomba serikali kufuta msamaha wa kodi kwa taasisi za kidini.
Reviewed by Zero Degree
on
10/07/2016 06:47:00 PM
Rating: