Loading...

Rais wa Colombia ashinda Tuzo ya AMANI ya Nobel.


Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo amani ya Nobel kwa mwaka 2016 kutokana na juhudi zake za kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya nusu karne.



“Rais Santos alianzisha majadiliano yaliopelekea kusainiwa kwa mkataba kati ya serikali ya Colombia na waasi wa kundi la FARC, na amekuwa akifanya juhudi za kupeleka mbele mchakato wa amani,” ilisema kamati hiyo katika taarifa yake.
Vita vya wenyewe kwa wenye nchini Colombia ambavyo ni mmoja ya vita vya muda mrefu zaidi katika zama hizi, vimegharimu maisha ya Wacolombia wasiopungua 220,000 na kuwakosesha makazi watu wapatao milioni 6.

Tuzo hiyo yenye thamani ya dola 930,000, ilitolewa wakfu na mwanaviwanda wa Sweden na mgunduzi wa baruti Alfred Nobel. Mwaka uliyopita kundi la pande nne la majadiliano la Tunusia ambalo ni muungano wa vyama vya wafanyakazi, mashirika ya watoa ajira, makundi ya haki za binaadamu na mawakili walishinda tuzo hiyo.


ZeroDegree.
Rais wa Colombia ashinda Tuzo ya AMANI ya Nobel. Rais wa Colombia ashinda Tuzo ya AMANI ya Nobel. Reviewed by Zero Degree on 10/07/2016 06:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.