Loading...

Rais Barack Obama amtaka Trump aache kulalama kwamba anafanyiwa hila.

Rais Barack Obama wa Marekani amemshutumu mgombea Urais nchini humo kupitia chama cha Republican Donald Trump kwa madai anayotoa kwamba kuna hila dhidi yake zinazofanywa katika uchaguzi nchini humo, na kumtaka kuacha kulalama.

Amesema malalamiko ya mgombea huyo ni jambo ambalo halijawahi kutokea kwa mgombea nchini Marekani kujaribu kutilia shaka uchaguzi hata kabla haujafanyika.

'' Sijawahi kuona katika maisha yangu ama katika historia za siasa za sasa kwa mgombea yoyote wa kiti cha Urais kujaribu kujaribu kutilia shaka uchaguzi na taratibu za uchaguzi kabla ya zoezi la upigaji kura kufanyika. Na hakuna ukweli wowote'' alisema Rais Obama.


Rais Barack Obama.
Aidha Rais Obama amempa ushauri Mgombea huyo wa Republican ambaye ni mfanyabiashara tajiri Donald Trump kuendelea na kile anachokitafuta kuwa Rais ajaye wa Marekani.

''...Namshauri Bwana Trump kuacha kulalamika na kujaribu kuchukulia suala lake hilo kujaribu kupata kura. Na kama atapata kura nyingi hivyo itakuwa matarajio yangu kwa Hilary Clinton kutoa hotuba na kutaka kufanya naye kazi kwa ajili ya juhakikisha kwamba watu wa Matrekani wananufaika na serikali. Na itakuwa ni kazi yangu kumkaruibisha Bwana Trump bila kujali alichosema kuhusu mimi ama tofauti yangu dhidi yake juu ya mawazi yangu na pia kumsindikiza kuweza kukabidhiana madaraka kwa amani. Hivyo ndivyo Wamarekani wanavyofanya...'' Alisema Rais Obama

Rais wa Marekani pia amemlaumu Bwana Trump kuonesha kwake kumsifu Rais wa Urusi Vladmir Putin na sera zake kufuata za kiongozi huyo.

Kampeni za Uchaguzi nchini Marekani zimekuwa zikifanyika katika hatua za lala salama, ikiwa imebaki siku chahe kufanyika kwake. huku Donald Trump akiendelea kuwaambia wafuasi wake kwamba serikali ya nchi hiyo, imekuwa ikimchafua lakini atashinda.


Credits: BBC Swahili
ZeroDegree.
Rais Barack Obama amtaka Trump aache kulalama kwamba anafanyiwa hila. Rais Barack Obama amtaka Trump aache kulalama kwamba anafanyiwa hila. Reviewed by Zero Degree on 10/19/2016 08:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.