Loading...

Rais Magufuli alekea Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo ameagwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa safari yake ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili. Hii ni safari yake rasmi ya tatu kwenda nje ya nchi toka aingie madarakani mwaka mmoja uliopita. Alisafiri kwa mara ya kwanza alikwenda Rwanda, kisha akaenda Uganda.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa safari hiyo mapema leo.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Balozi wa Kenya nchini Mhe Boniface Muhia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Inspekta jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wakati akipanda ndege kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016.


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine wakipunga mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akianza safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016.

Magufuli alakiwa na waziri wa mambo ya nje.


Wizara ya mambo ya nje Kenya imepakia picha za Rais Magufulia kilakiwa uwanja wa ndege na waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohamed. Bi Mohamed anawania wadhifa wa rais wa tume ya Umoja wa Afrika (AU).


Rais Magufuli na Bi Amina Mohamed.

ZeroDegree.
Rais Magufuli alekea Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili. Rais Magufuli alekea Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili. Reviewed by Zero Degree on 10/31/2016 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.