Loading...

Samatta atangazwa na Shirikisho la soka la Africa [ CAF ] kuwania tuzo za mchezaji bora wa mwaka.

NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ni miongoni mwa wachezaji 30 waliotangazwa na Shirikisho la Soka la Afrika(CAF) kuwania tuzo za mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika.

Samatta, ambaye ni mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wa ndani kwa msimu uliopita, ameteuliwa kushindania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika kutokana na kiwango bora anachoonesha akiwa na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.



Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na TP Mazembe, amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake ya KRC Genk ambapo aliifungia timu hiyo mabao muhimu yaliyoiwezesha kuingia kwenye mechi za mchujo za mashindano ya Europa na kisha kuiwezesha kufuzu kuingia kwenye hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa mtandao wa CAF jana, Samatta anaungana na wachezaji wengine wawili kutoka Afrika Mashariki kuwania tuzo hiyo wachezaji hao ni Victor Wanyama kutoka Kenya anayekipiga kwenye klabu ya Tottenham Hotspurs ya England na kipa wa kimataifa wa Uganda, Dennis Onyango wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Wanyama amekuwa na msimu mzuri kwenye klabu ya Southampton na kumpatia nafasi ya kusajiliwa kwenye klabu ya Tottenham Hotspurs msimu huu na Dennis Onyango aliiongoza Uganda kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika lakini pia ameiongoza Mamelodi Sundowns kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Mbali na Samatta wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo yupo mwanasoka bora wa msimu uliopita wa Afrika, Pierre Emerick Aubameyang kutoka Gabon ambae anaichezea Borrusia Dortmund ya Ujerumani, Riyahd Mahrez (Algeria, Leicester City), Islam Sliman(Algeria, Leicester City).

Orodha kamili ya wanaowania tuzo hiyo ni Riyad Mahrez (Algeria, Leicester City) El Arabi Hillel Soudani (Algeria, Dinamo Zagreb), Islam Slimani (Algeria , Leicester City) Samuel Eto’o (Cameroon, Antalyaspor), Benjamin Mounkandjo (Cameroon na Lorient).

Serge Aurier (Ivory Coast, PSG), Eric Bailly (Ivory Coast, Manchester City), Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Ivory Coast, Hebei Fortune), Mohamed Salah (Misri, Roma), Mohamed El Neny (Misri, Arsenal), Pierre Emerick Aubameyang (Gabon, Dortmund).

Andre Ayew (Ghana, West Ham), Victor Wanyama (Kenya, Tottenham), William Jebor (Liberia, Wydad Athletic Club), Mehdi Benatia (Morocco & Juventus), Hakim Ziyech (Morocco, Ajax), John Mikel Obi (Nigeria, Chelsea), Kelechi Iheanacho (Nigeria, Manchester City), Ahmed Musa (Nigeria , Leicester City).

Cedric Bakambu (DR Congo, Villareal), Yannick Bolasie (DR Congo, Everton), Sadio Mane (Senegal, Liverpool) , Kalidou Koulibaly (Senegal, Napoli), Keegan Dolly (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns), Itumeleng Khune (Afrika Kusini, Kaizer Chiefs).

Mbwana Samatta (Tanzania, Genk), Aymen Abdennour Tunisia, Valencia), Wahbi Khazri (Tunisia, Sunderland), Dennis Onyango (Uganda, Mamelodi Sundowns), Khama Billiat (Zimbabwe, Mamelodi Sundowns).

ZeroDegree.
Samatta atangazwa na Shirikisho la soka la Africa [ CAF ] kuwania tuzo za mchezaji bora wa mwaka. Samatta atangazwa na Shirikisho la soka la Africa [ CAF ] kuwania tuzo za mchezaji bora wa mwaka. Reviewed by Zero Degree on 10/16/2016 02:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.