Loading...

Serikali kusomesha mtoto wa mtafiti aliyeuawa.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha ameongoza waombolezaji kwenye maziko ya aliyekuwa mtafiti wa maabara ya udongo ya Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian, Teddy Lumanga yaliyofanyika Olasiti jijini hapa.

Akitoa salamu za Serikali jana, Nasha alisema baada ya Serikali kupata taarifa kuwa Lumanga aliomba kwa bidii apate safari ya kikazi ili imwezeshe kupata ada ya mtoto wake, imeamua kugharimia elimu yake hadi atakapohitimu.


Alisema tukio la watafiti hao kuuawa kikatili limeisononesha Serikali, kwani walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi.

Ibada ya mazishi ilifanyika kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti, Jimbo Kuu la Arusha, ambako Padri Augustine Temu alisema wao na familia wanapaswa kuwasamehe waliotenda ukatili wa kuwaua watafiti hao na kuiachia Serikali ifanye uchunguzi na kuwachukulia hatua.

ZeroDegree.
Serikali kusomesha mtoto wa mtafiti aliyeuawa. Serikali kusomesha mtoto wa mtafiti aliyeuawa. Reviewed by Zero Degree on 10/05/2016 09:38:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.