Loading...

Suarez kulipwa milioni 700 kwa wiki.

MKATABA mpya atakaopewa hivi karibuni pale Camp Nou utamfanya Luis Suarez kuingiza mshahara mnono kama ule anaopokea staa mwenzake Neymar.

Mkataba wa sasa wa Suarez na mabingwa hao wa La Liga na Ulaya utafikia tamati mwaka 2019 na hivi sasa analipwa pauni 170,000 kwa wiki.


Kwa mujibu wa taarifa, Suarez anatarajia kusaini mkataba mpya na Barcelona hivyo atapata ongezeko la kitita cha pauni 100,000 katika mshahara wake huo wa sasa.

Suarez na Neymar watakuwa wakiweka mfukoni pauni 272,000 (zaidi ya Sh milioni 700) kila mmoja na kwa mshahara huo watakuwa wamezidiwa na Lionel Messi pekee anayekinga pauni 360,000, ambazo ni zaidi ya bilioni 900 za Kitanzania.

Gazeti la Catalonia la Hispania limenyetisha kuwa Barca wanataka kumpa Suarez mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuvutiwa na ‘mavituzi’ yake uwanjani.

Tangu alipotua Catalunya mwaka 2014 akitokea Liverpool, straika huyo wa kimataifa wa Uruguay amekuwa moto wa kuotea mbali.

Kwa kiasi hicho cha fedha, Suarez amewapiku Andres Iniesta na Sergio Busquets ambapo anaingiza mara mbili ya mshahara wanaopokea Wahispania hao.

Nyota hao waliotokea katika ‘academy’ ya Barca, La Masia, wanakinga pauni 136,000 kwa wiki.

Anayefuata katika orodha hii ni kiungo wa Croatia, Ivan Rakitic ambaye mkataba wake wa sasa unamtaka kuvuna pauni 110,000 kwa wiki.

Gerard Pique aliyeiwezesha klabu hiyo kunyakua mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, anachukua pauni 98,000 kila baada ya wiki moja.

Jordi Alba na Arda Turan ni miongoni mwa mastaa wa klabu hiyo wanaopokea mshahara kiduchu ambapo kila mmoja analipwa pauni 68,000 kwa wiki.

ZeroDegree.
Suarez kulipwa milioni 700 kwa wiki. Suarez kulipwa milioni 700 kwa wiki. Reviewed by Zero Degree on 10/06/2016 05:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.