Loading...

Umoja wa Afrika [ AU ], wamuenzi Mwalimu Nyerere.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amezindua jengo jipya la makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) ambalo limepewa jina la Baba wa Taifa la Tanzania, Julius Nyerere.

Kuzinduliwa kwa jengo hilo jijini Adis Abba Ethiopia na Kansela Angela ambaye yuko barani Afrika kwa ziara yake ya kikazi, kunafuatia mkakati ulionzishwa na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe wakati akiwa mwenyekiti wa umoja huo akisisitiza haja ya kuenzi mchango uliotolewa na Mwalimu Nyerere kwa nchi za Afrika.

Akizungumza kwenye mkutano wa AU miaka michache iliyopita, Rais Mugabe alimsifu Nyerere kama mwanamapinduzi wa kweli wa Afrika aliyesaulika kuenziwa.

Aliutaka AU kutambua mchango wa Nyerere wakati wa uhai wake kwa kujenga jengo maalumu.

Kuzinduliwa kwa jengo hilo, kunakuwa ni mara ya kwanza kwa makao makuu ya umoja huo kutambua mchango wa waasisi wa Afrika.

Jengo hilo ambalo jina lake kamili ni Jengo la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Ujerumani.

Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na kutumiwa na maofisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.

Ujenzi wa jengo hilo ambalo linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu Euro 27 milioni.

Wakati wa utawala wake, Nyerere alitoa mchango mkubwa kupigania uhuru kwa baadhi ya nchi zilizopo kusini mwa Afrika kupata uhuru wake. Miongoni mwa nchi hizo ni Angola, Namibia, Msumbiji na Zimbambwe.

Nyerere pia alishiriki kupinga utawala wa ubaguzi wa Afrika Kusini.

ZeroDegree.
Umoja wa Afrika [ AU ], wamuenzi Mwalimu Nyerere. Umoja wa Afrika [ AU ], wamuenzi Mwalimu Nyerere. Reviewed by Zero Degree on 10/12/2016 08:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.