Loading...

Video: Goli lililovunja rekodi ya Dunia katika mashindano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018.

Striker wa Crystal Palace Christian Benteke ameweka historia usiku wa October 10 kwa kufunga goli sekunde ya 7 baada mchezo kuanza wakati Ubelgiji ikicheza dhidi ya Gibraltar.

Romelu Lukaku alikosekana kwenye mchezo huo kutokana na majeraha, na kutoa nafasi kwa Benteke ambaye ameweka rekodi yake kwa kuwa mchezaji aliyefunga goli la mapema zaidi kwenye historia ya hatua za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Davide Gualtieri wa San Marino alikuwa anashikilia rekodi hiyo baada ya kufunga goli sekunde ya 8.3 dhidi ya England November 1993.

Christian Benteke aliyeshindwa kutamba kwenye kikosi cha Liverpool liinasa pasi ya mchezaji wa Gibraltar kisha kabla ya kufunga bao kwa mguu wa kushoto.

Aliongeza bao jingine dakika mbili kabla ya mapumziko na kuifanya Ubelgiji kuwa mbele kwa magoli 3-0 hadi wakati wa mapumziko.

Benteke alikamilisha hat trick yake 55 kipindi cha pili katika mchezo huo ambao Ubelgiji ilishinda kwa magoli 6-0.

Wafungaji wengine wa magoli ya Ubelgiji ni Witsel (19’), Mertens (51’) na Hazard (79).





ZeroDegreee.
Video: Goli lililovunja rekodi ya Dunia katika mashindano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018. Video: Goli lililovunja rekodi ya Dunia katika mashindano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018. Reviewed by Zero Degree on 10/11/2016 10:06:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.